Hamia kwenye habari

Kushoto: Kimbunga Helene kwenye Ghuba ya Mexico, Septemba 26, 2024. Juu kulia: Jumba la Ufalme lililoathiriwa na mafuriko katika mji wa Swannanoa, North Carolina, Marekani. Chini kulia: Nyumba ya ndugu ambayo imefunikwa na miti katika mji wa Asheville, North Carolina

OKTOBA 3, 2024
MAREKANI

Kimbunga Helene Chasababisha Uharibifu Kusini-Mashariki mwa Marekani

Kimbunga Helene Chasababisha Uharibifu Kusini-Mashariki mwa Marekani

Septemba 26, 2024, Kimbunga Helene kilifika kwenye pwani ya Florida, Marekani. Kimbunga hicho chenye nguvu kilisababisha mvua kubwa yenye upepo mkali uliofikia kilomita 225 kwa saa. Septemba 27, kimbunga hicho kiliingia Georgia na kusababisha upepo mkali wa kilomita 95 kwa saa. Siku iliyofuata, kimbunga hicho kilielekea kaskazini na kuingia South Carolina, ambapo kilisababisha angalau vimbunga vingine vitatu. Kimbunga Helene kilipofika North Carolina, mvua ya kiwango cha sentimita 90 ilinyesha katika majiji kadhaa.

Upepo mkali na mvua kubwa vilivyotokana na Kimbunga Helene vilisababisha mafuriko na uharibifu mkubwa wa nyumba, biashara, na barabara. Zaidi ya watu milioni moja waliachwa bila umeme. Watu 180 hivi walikufa.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Kwa kusikitisha, ndugu 3 walikufa

  • Wahubiri 7 walipata majeraha madogo

  • Wahubiri 1,606 walilazimika kuhama makazi yao

  • Nyumba 29 ziliharibiwa kabisa

  • Nyumba 236 zilipata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 779 zilipata uharibifu mdogo

  • Jumba 1 la Ufalme lilipata uharibifu mkubwa

  • Majumba 19 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Waangalizi wa mzunguko na wazee wa eneo hilo, wanaendelea kushughulikia mahitaji ya kiroho na ya kimwili ya walioathiriwa na kimbunga hicho

  • Halmashauri 2 za Kutoa Msaada zinasimamia jitihada za kutoa msaada.

Tunasikitishwa na vifo vilivyosababishwa na kimbunga hicho. Hata hivyo, tunapata faraja na amani kutokana na ahadi za Yehova kwamba wakati ujao kila mtu “ataishi kwa usalama naye hatahangaishwa na woga wa msiba.”​—Methali 1:33.