Hamia kwenye habari

Ndugu Jovidon Bobojonov

MACHI 31, 2020
TAJIKISTAN

Ndugu Jovidon Bobojonov Anaweza Kuhukumiwa Kifungo cha Gerezani kwa Sababu ya Kukataa Utumishi wa Kijeshi Nchini Tajikistan

Ndugu Jovidon Bobojonov Anaweza Kuhukumiwa Kifungo cha Gerezani kwa Sababu ya Kukataa Utumishi wa Kijeshi Nchini Tajikistan

Jumatano, Aprili 1, 2020, mahakama ya kijeshi ya Tajik, iliyo katika mji mkuu wa Dushanbe itatoa hukumu juu ya kesi ya Ndugu Jovidon Bobojonov kwa kuwa amekataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri. Kwa zaidi ya miezi mitano, Ndugu Bobojonov amekuwa akisubiri uamuzi huo wa mahakama huku akivumilia hali ngumu.

Oktoba 4, 2019, maofisa wa jeshi jijini Khujand walimchukua kwa lazima Ndugu Bobojonov mwenye umri wa miaka 19 akiwa nyumbani na kumpeleka katika ofisi ya uandikishaji, ambako aliwekwa chini ya ulinzi. Baada ya siku mbili alipandishwa treni kwa lazima na kupelekwa kwenye kituo cha mazoezi ya kijeshi iliyo katika wilaya ya Lenin. Kisha akawekwa kwenye kitengo namba Na. 45075 ambako maofisa walijaribu kumlazimisha avae mavazi ya kijeshi na kutoa kiapo cha utii. Januari 28, 2020, kesi ya uhalifu ikafunguliwa dhidi yake.

Wazazi wa Jovidon ambao ni Mashahidi pia, wamewasilisha malalamiko yao kwa watu mbalimbali wenye mamlaka Tajikistan, kutia ndani Ofisi ya Rais na Ofisi ya Ombudsman. Wenye mamlaka hao nchini Tajik wanadai kwamba, kwa kuwa sheria ya utumishi mbadala wa kiraia iliyowekwa, bado haijaanza kutumiwa, basi tendo la Bw. Bobojonov la kukataa utumishi wa kijeshi ni la kihalifu, na kwamba tendo la kumchukua kwa lazima halikuwa kinyume na sheria.

Tunajua kwamba Yehova atambariki Ndugu Bobojonov kwa ujasiri wake na kumpa yeye pamoja na familia yake nguvu na amani.—Zaburi 29:11.