MEI 19, 2022 | HABARI ZILIONGEZWA: FEBRUARI 6, 2023
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU | Imani Yajaribiwa Huko Lesozavodsk
Februari 3, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Lesozavodskiy iliyo katika Eneo la Primorye iliwahukumu Ndugu Yevgeniy Grinenko na Ndugu Sergey Kobelev pamoja na Dada Svetlana Yefremova. Yevgeniy na Sergey walihukumiwa kifungo cha nje cha miaka sita. Svetlana alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka mitatu. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.
Mfuatano wa Matukio
Mei 12, 2020
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Yevgeniy kwa sababu wenye mamlaka walidai kwamba alihusika katika k upanga utendaji wa kikundi chenye msimamo mkali. Maofisa wa FSB waliagizwa kufanya msako katika nyumba ya Yevgeniy na nyumba ya Sergey. Maofisa wengine walienda kazini kwa Sergey na kumkamata. Sergey alihojiwa kwa saa nne na kuachiliwa. Yevgeniy pia alikamatwa na kuwekwa kizuizini
Mei 14, 2020
Mahakama iliamuru kwamba Yevgeniy awekwe mahabusu
Mei 29, 2020
Wenye mamlaka walimhamisha Yevgeniy na kumpeleka kwenye mahabusu katika eneo la Spassk-Dalny
Julai 8, 2020
Mahakama ilimwachilia Yevgeniy kutoka mahabusu na kumweka katika kifungo cha nyumbani
Februari 6, 2021
Yevgeniy aliachiliwa kutoka kwenye kifungo cha nyumbani na akaagizwa asiondoke kwenye eneo hilo
Machi 8, 2021
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Sergey kwa sababu wenye mamlaka walidai kwamba alishiriki katika utendaji wa shirika lenye msimamo mkali
Aprili 6, 2021
Svetlana aliongezwa kwenye kesi hiyo
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Ndugu na dada zetu waaminifu wametuwekea mfano mzuri wa kuwa jasiri wanapoingia “katika Ufalme wa Mungu kupitia dhiki nyingi.”—Matendo 14:22.