Hamia kwenye habari

Ndugu Yevgeniy Spirin na mke wake, Natalya

OKTOBA 14, 2020
URUSI

Mahakama ya Rufaa ya Urusi Yaunga Mkono Kifungo na Faini Dhidi ya Ndugu Spirin

Mahakama ya Rufaa ya Urusi Yaunga Mkono Kifungo na Faini Dhidi ya Ndugu Spirin

Oktoba 14, 2020, Mahakama ya Eneo la Ivanovo iliunga mkono kifungo na faini ya awali iliyotolewa Julai 2020 dhidi ya Ndugu Yevgeniy Spirin. Mahakama ya rufaa ya eneo hilo ilikataa ombi la mwendesha-mashtaka kwamba kesi ya Ndugu Spirin isikilizwe upya. Kuna uwezekano mkubwa kwamba mwendesha-mashtaka atakata rufaa uamuzi huu na kuomba mahakama ikubali ombi lake la awali la kumfunga Ndugu Spirin kwa miaka saba.