Hamia kwenye habari

Kushoto hadi kulia: Dada Silaeva, Dada Shamsheva, Ndugu Khokhlov, na Ndugu Zhinzhikov wakiwa mahakamani Oktoba 28, 2020

OKTOBA 28, 2020
URUSI

Mahakama ya Urusi Yaunga Mkono Kifungo cha Ndugu Wawili na Dada Wawili

Mahakama ya Urusi Yaunga Mkono Kifungo cha Ndugu Wawili na Dada Wawili

Oktoba 28, 2020, Mahakama ya Eneo la Bryansk iliunga mkono kifungo cha Ndugu Vladimir Khokhlov, Ndugu Eduard Zhinzhikov, Dada Tatyana Shamsheva, na Dada Olga Silaeva. Awali walihukumiwa vifungo vya mwaka mmoja hadi mwaka mmoja na miezi mitatu gerezani. Hata hivyo, kwa kuwa tayari walikuwa wamefungwa mahabusu, hawakuhitaji kwenda gerezani. Hukumu iliyotolewa leo inamaanisha kwamba wataendelea kutambuliwa kuwa wahalifu waliowahi kufungwa. Hata hivyo, wanafurahi kwamba wataendelea kuwa huru kwa kuwa hakuna msingi wa mwendesha-mashtaka kukata rufaa na kuomba wapewe hukumu kali zaidi.

Kabla ya kifungo chao cha awali, akina ndugu walitumia siku 316 mahabusu na akina dada walikuwa mahabusu kwa siku 245. Baada ya kuachiliwa, akina dada hao walihojiwa katika Ripoti ya 5 ya Baraza Linaloongoza ya 2020. Walisema kwamba kusali, kusoma Biblia, na kuendelea kuwa na roho ya shukrani kuliwasaidia kuvumilia kwa shangwe.