Hamia kwenye habari

Ndugu Sergey Rayman na mke wake, Valeriya, wakiwa mahakamani Oktoba 9, 2020

OKTOBA 9, 2020
URUSI

Mahakama ya Urusi Yawahukumu Wenzi wa Ndoa Vijana Kifungo cha Nje

Mahakama ya Urusi Yawahukumu Wenzi wa Ndoa Vijana Kifungo cha Nje

Oktoba 9, 2020, Mahakama ya Wilaya ya Sverdlovskiy katika jiji la Kostroma ilimhukumu Ndugu Sergey Rayman na mke wake, Valeriya. Sergey alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka nane na Valeriya akahukumiwa kifungo cha miaka saba. Hivyo ndivyo vifungo virefu zaidi vya nje ambavyo ndugu na dada yeyote amehukumiwa nchini Urusi tangu uamuzi wa Mahakama Kuu mwaka wa 2017. Ndugu na Dada Rayman hawatahitaji kwenda mahakamani wakati huu.