Mazungumzo ya Familia
Mazungumzo ya Familia
Kuna Kasoro Gani Katika Picha Hii?
Soma Yohana 6:5-13. Ni mambo gani matatu katika picha hii ambayo si sahihi? Andika majibu yako kwenye mistari iliyo hapa chini na ukamilishe picha hii kwa kuipaka rangi.
1. ․․․․․
2. ․․․․․
3. ․․․․․
ZUNGUMZENI PAMOJA:
Yesu aliwaambia wanafunzi wake wakusanye nini, na kwa nini? Hilo linakufundisha nini kumhusu Yesu? Unaweza kufanya nini ili uepuke hasara?
UTENDAJI WA FAMILIA:
Someni simulizi hilo la Biblia pamoja. Ikiwezekana, mmoja asome sehemu ya msimuliaji, wa pili asome sehemu ya Yesu, wa tatu asome sehemu ya Filipo, na wanne asome sehemu ya Andrea.
Kusanya na Ujifunze
Kata, kunja katikati, na uhifadhi
KADI YA BIBLIA 1 YOSHUA
MASWALI
A. Yoshua na jeshi lake waliangusha kuta za Yeriko kwa njia gani?
B. Kamilisha sentensi hii ya Yoshua: “Mimi na nyumba yangu, . . .”
C. Yoshua alijulikana kwa majina gani mengine?
[Chati]
4026 K.W.K. 1 W.K. 98 W.K.
Adamu aumbwa Aliishi miaka ya Kitabu cha mwisho
1500 K.W.K. cha Biblia kinaandikwa
[Ramani]
Alihama kutoka Misri kwenda kwenye Nchi ya Ahadi
MISRI
NCHI YA AHADI
YOSHUA
MAMBO MACHACHE KUMHUSU
Mwana wa Nuni. Alikuwa mtumishi wa Musa na baadaye akawekwa rasmi kuongoza Israeli. (Kutoka 33:11; Kumbukumbu la Torati 34:9; Yoshua 1:1, 2) Yoshua aliwaongoza watu wa Mungu bila woga waingie katika Nchi ya Ahadi. Alitumaini ahadi za Yehova, akatii mwongozo wake, na kumtumikia kwa uaminifu.
MAJIBU
A. Walimtii Mungu kwa kuzunguka jiji hilo.—Yoshua 6:1-27.
B. “. . . tutamtumikia Yehova.”—Yoshua 24:15.
C. Hoshea na Yehoshua.—Hesabu 13:8, 16.
Watu na Nchi
4. Jina langu ni Victor. Nina umri wa miaka 7 na ninaishi nchini Malawi, barani Afrika. Kuna Mashahidi wangapi wa Yehova nchini Malawi? Ni 750, 7,500, au 75,000?
5. Ni nukta gani inayoonyesha eneo ninamoishi. Chora duara kuizunguka na utie nukta kuonyesha eneo unaloishi kisha uone kwenu ni umbali gani kutoka Malawi.
A
B
C
D
Watoto Watafute Picha
Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.
● Majibu ya ukurasa wa 30 na 31 kwenye ukurasa wa 22
MAJIBU YA UKURASA WA 30 NA 31
1. Chakula hicho kinapaswa kubebwa na mvulana, si msichana.
2. Kunapaswa kuwa na mikate mitano, si matofaa matano.
3. Kunapaswa kuwa na samaki wawili, si mahindi mawili.
4. 75,000.
5. C.