Mazungumzo Ya Familia
Mazungumzo Ya Familia
Kuna Tofauti Gani?
Unaweza kutambua tofauti tatu kati ya picha A na B? Andika majibu yako kwenye mistari iliyo hapo chini, na ukamilishe picha hizo kwa kuzipaka rangi.
DOKEZO: Soma Kutoka 25:23, 30, 31, 37; 30:1-7; Mambo ya Walawi 24:5, 6.
1. ․․․․․
2. ․․․․․
3. ․․․․․
4. Ni picha gani iliyo sahihi, picha A au picha B?
ZUNGUMZENI PAMOJA:
Makuhani walipaswa kufanya nini kabla ya kuanza kufanya kazi katika maskani?
DOKEZO: Soma Kutoka 30:17-21.
Ikiwa unataka kumfurahisha Yehova na wazazi wako, ni muhimu kadiri gani uwe safi? Zaidi ya kuwa safi kimwili, unaweza kuwa safi kwa njia gani nyingine?
DOKEZO: Soma 1 Wakorintho 6:9-11; 2 Wakorintho 7:1.
UTENDAJI WA FAMILIA:
Kila mtu katika familia afanye utafiti kuhusu “Mahali Patakatifu” katika maskani. (Waebrania 9:2) Kisha mkutane na kila mmoja aeleze jambo moja jipya ambalo amejifunza.
DOKEZO: Soma Zaburi 119:105; 141:2; Mathayo 4:4; Yohana 4:34; Ufunuo 8:4.
Kusanya na Ujifunze
Kata, kunja katikati, na uhifadhi
KADI YA BIBLIA 9 YEREMIA
MASWALI
A. Yehova alimtumia Yeremia kuandika vitabu gani vinne vya Biblia?
B. Kweli au si kweli? Yeremia alibaki akiwa mseja.
C. Kamilisha maneno haya ya Yeremia: “Moyoni mwangu [neno la Mungu] likawa kama . . . ”
[Chati]
4026 K.W.K. 1 W.K. 98 W.K.
Adamu aumbwa Aliishi miaka Kitabu cha mwisho
ya 650 K.W.K. cha Biblia
kinaandikwa
[Ramani]
Aliishi Yerusalemu. Akasafiri hadi Mto Efrati na Misri—Yeremia 13:1-9; 43:8-13
Yerusalemu
Efrati
MISRI
YEREMIA
MAMBO MACHACHE KUMHUSU
Alichaguliwa awe nabii kabla ya kuzaliwa. (Yeremia 1:1-5) Yeremia alimtumikia Mungu kwa uaminifu kwa zaidi ya miaka 65. Ingawa Yeremia alihisi kwamba hakuwa na uzoefu na aliogopa kusema, Yehova alimwambia: “Usiogope . . . , kwa maana ‘mimi niko pamoja nawe ili kukukomboa.’”—Yeremia 1:6-8.
MAJIBU
A. Kitabu cha Kwanza na cha Pili cha Wafalme, Yeremia, na Maombolezo.
B. Kweli.—Yeremia 16:1-4.
C. “. . . moto unaowaka ambao umefungiwa ndani ya mifupa yangu.”—Yeremia 20:9.
Watu na Nchi
5. Jina langu ni Geoffrey. Nina umri wa miaka tisa, na ninaishi Fiji. Kuna Mashahidi wangapi wa Yehova nchini Fiji? Ni 500, 2,500, au 10,500?
6. Ni alama gani inayoonyesha eneo ninaloishi? Chora duara kuzunguka alama hiyo, na uchore alama nyingine kuonyesha eneo unaloishi kisha uone kwenu ni umbali gani kutoka Fiji.
A
B
C
D
Watoto Watafute Picha
Je, unaweza kupata picha hizi katika toleo hili? Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jambo linalotendeka katika kila picha.
● Majibu ya “MAZUNGUMZO YA FAMILIA” yanapatikana kwenye ukurasa wa 27
MAJIBU YA UKURASA WA 30 NA 31
1. Idadi ya taa kwenye kinara cha taa.
2. Idadi ya mikate ya wonyesho.
3. Pembe zilizotokea kwenye madhabahu ya uvumba.
4. A.
5. 2,500.
6. D.