Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Jino Linalojinoa la Mwanamizi wa Baharini

Jino Linalojinoa la Mwanamizi wa Baharini

Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Jino Linalojinoa la Mwanamizi wa Baharini

● Kwa kutumia meno yake matano, mwanamizi hutoboa mwamba ili kutengeneza nyumba ya kujificha. Licha ya kusaga na kukwangura, makali ya meno ya mwanamizi huwa hayaishi. “Hakuna kifaa kingine tunachojua kinachoweza kufanya hivyo, iwe ni cha kukatia au kusagia,” anasema Pupa Gilbert, profesa wa fizikia katika Chuo Kikuu cha Wisconsin–Madison nchini Marekani. Siri ya mwanamizi ni nini?

Fikiria hili: Jino la mwanamizi lina chembechembe ambazo zimeunganishwa pamoja. “Meno yake yana matabaka yaliyoachana yanayoweza kuvunjika inapohitajika,” anasema Gilbert. Ni rahisi kwa tabaka lililochakaa la jino kudondoka na kuacha tabaka jipya lenye makali kwa kuwa maeneo kati ya matabaka mawili huwa na chembechembe dhaifu. Kwa kuwa upande mmoja wa jino hilo huendelea kuota na wakati huohuo ule upande mwingine ukiendelea kujinoa, halitawahi kuwa butu. Gilbert analiita jino la mwanamizi “mojawapo ya maumbile machache ambayo hujinoa.”

Kujua jinsi jino la mwanamizi linavyojinoa kumewasisimua sana watu wanaotengeneza vifaa mbalimbali. Huenda ujuzi huo ukawasaidia kutengeneza vifaa vinavyoweza kujinoa kadiri vinavyotumiwa. “Siri ni kuchunguza mbinu inayotumiwa na mwanamizi,” anasema Gilbert.

Una maoni gani? Je, jino linalojinoa la mwanamizi lilijitokeza lenyewe? Au lilibuniwa?

[Mchoro katika ukurasa wa 16]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Jino linaloota

Bamba la kichokaa

Jino lililonolewa

[Picha katika ukurasa wa 16]

Mwanamizi

[Picha katika ukurasa wa 16]

Meno matano

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 16]

Both photos: Courtesy of Pupa Gilbert/University of Wisconsin-Madison