Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

KUUTAZAMA ULIMWENGU

Kumulika Mazingira

Kumulika Mazingira

Ingawa dunia hutoa hewa safi, chakula kizuri, na maji safi, wanadamu bado wanazidi kuharibu utendaji huo wa asili. Wanasayansi wanaendelea kujitahidi kutafuta njia za kutunza mazingira.

Australia

Imekadiriwa kwamba zaidi ya kilomita 500,000 za maji yasiyo na chumvi yako chini ya sakafu ya bahari ulimwenguni. Vincent mtaalamu wa elimu ya maji wa Chuo Kikuu cha Flinders, Adelaide, anasema hivi: “Kuna wakati ambapo usawa wa bahari ulikuwa chini zaidi kuliko vile ilivyo sasa hivi,” hivyo ufuo uliokuwepo wakati huo umemezwa na maji. Wakati huo, “Mvua ingejaza maji mpaka sehemu ya eneo ambalo kwa sasa liko chini ya bahari.” Wanasayansi wanatumaini kwamba kuhifadhiwa kwa sehemu hizo za chini ya bahari huenda kungesaidia watu zaidi ya milioni 700 ambao hawawezi kupata maji safi na salama.

Jangwa la Sahara

Nusu ya idadi ya jamii ya wanyama wakubwa waliokuwa wakipatikana katika jangwa la Sahara wametoweka au kubakia kwa asilimia moja au chini zaidi ya idadi yao ya mwanzoni. Misukosuko ya nchi na uwindaji wa wanyama ulioenea huchangia kupungua kwa wanyama hao. Ingawa jamii kubwa ya viumbe hai walio katika jangwa hukosa misitu, watafiti husema kwamba “kushindwa kwa wanasayansi kuwatunza viumbe hai walio katika jangwa husababishwa na kukosa misaada ya kifedha.” Matokeo ni kwamba, ni vigumu kwa wanaohifadhi mazingira kuwatunza viumbe wanaoishi jangwani walio katika hatari ya kutoweka.

Ulimwengu

Imekadiriwa kwamba kifo 1 kati ya 8 vilivyotokea mwaka 2012 kilisababishwa na uchafuzi wa hali ya hewa. Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni, “uchafuzi wa hali ya hewa ni tatizo kubwa la mazingira ulimwenguni linalohatarisha afya.”