WIMBO NA. 96
Kitabu cha Mungu Ni Hazina
-
1. Kuna kitabu ambacho huwapa,
Watu amani na tumaini.
Mawazo yake yana nguvu nyingi;
Kinafumbua macho ya watu.
Ni Biblia takatifu ya Mungu.
Iliandikwa kale na watu.
Waliompenda sana Yehova,
Walichochewa na roho yake.
-
2. Waliandika kuhusu ’umbaji,
Ulimwengu ulivyotokea.
Ukamilifu wa mtu mwanzoni.
Paradiso ilivyopotea.
Pia kuhusu malaika mwovu,
Aliyeipinga enzi kuu.
Kukawa dhambi, kifo, na huzuni,
Ushindi wa Yah waja upesi.
-
3. Leo twaishi pindi ya pekee.
Ufalme wa Mungu watawala.
Twatangaza habari za Ufalme,
Na baraka zitakazokuja.
Biblia inazo habari njema;
Ni karamu tele ya kiroho.
Huwapa watu wote tumaini;
Hiyo ni hazina kwelikweli.
(Ona pia 2 Tim. 3:16; 2 Pet. 1:21.)